Kwa darasa ya sanaa ya uchongaji, nitajenga ala ya muziki kutoka vitu anuwai. Ninasoma ala ya muziki kutoka afrika ya mashariki kujifunza zaidi kuhusu ala na kutengeneza ala. Ala nyingi zinatoka Kenya, Tanzania, Uganda, na nchi nyingi za afrika ya mashariki. Muziki ni muhimu sana kwa sherehe au kupitisha taarifa. Kwa mfano, muziki inatumika na harusi, mazishi, matibabu, kuweka saa, kufundisha, kufurahisha, na khadithia.
Embaire
Embaire iko ala ya kufanana na marimba na inatoka nchi ya Uganda. Kutengeneza embaire, tundu linachimbwa futi moja na nusu ya chini na urefu ni futi nane. Shina la ndizi linalazwa kwa upande pamoja wa tundu. Majani ya tembo marefu yanalazwa juu ya shina kama mto. Mbao (kutoka mbao ya ensambiya) za kufanana sehemu ya kinanda (piano) zinalazwa juu ya majani kuficha tundu. Embaire ina mbao ishirini na moja na watu wa sita hupiga embaire mara moja. Kupiga embaire, wanamuziki wanatumia fimbo/nyundo (kutoka mbao ya enzo) au mikono yao. Kwa watu wa Busoga, muziki ina uhusiano wa roho na desturi ya Mbusoga kutoa mhanga kuku kurekebisha sauti ya embaire.
Endere
Endere iko filimbi na inatoka Uganda pia. Endere ni fupi au refu na filimbi yote ina tundu la mraba nne. Endere fupi inatoka Uganda ya mashiriki na watu wa Busoga. Endere refu inatoka Uganda ya magharibi na watu wa Ankole. Kwa kawaida, endere inapigwa na mtu peke yake lakini karibuni watu wanapiga endere na ala za muziki zingine. Wachungaji walipiga endere kuita mifugo yao.
Endingidi
Endingidi ni kufanana na fidla lakini ina kamba moja. Sehemu ya endingidi inaweza kuondoshwa rahisi na watu wanaweza kuileta ala hii bila jasho. Kamba ya ala hii inatengenezwa na ufumwale ya makongo. Makongo inaotesha kabisa afrika ya mashariki. Mwanamuziki anapiga ala na upinde na inatengenezwa na ufumwale ya makongo pia. Kasha ya wazi inatumiwa kwa mwili wa ala. Kasha inajengwa na mbao kutoka mti wa settaala. Kasha ya juu inafunikwa na ngozi ya ng'ombe changa au mbuzi changa, lakini kwanza ngozi inaweka katika maji na baadaye inanyoshwa juu ya kasha. Ngozi inafungwa na nyundo na mambo juu ya kasha. Mpini ya endingidi unachongwa na mbao gumu. Mwanamuziki huweka nywele ya nyama juu ya endingidi kwa pambo. Ala hii inamalizika katika miezi tano au sita.
Ntongooli
Ntongooli (au ndongo) ni kufanana na Endingidi lakini ina kamba nane. Ala hii ina pia bakuli ya wazi kwa mwili wa ala. Bakuli inatoka kaka ya kobe na ngozi inawekwa juu ya bakuli. Mpini wa ntongooli unachongwa na mbao kama endingidi. Mtu anaanza kujenga ntongooli au endingidi na mpini. Mtu anachonga mpini kwa muda mrefu.
Kutazama wanamuziki wanapiga ala hizi...http://www.youtube.com/watch?v=ySP3VqcwWNI
http://www.youtube.com/watch?v=Xbrxxxx6qXA



No comments:
Post a Comment