Sunday, February 22, 2009

ALA YA MUZIKI YA AFRIKA YA MASHARIKI

Kwa darasa ya sanaa ya uchongaji, nitajenga ala ya muziki kutoka vitu anuwai. Ninasoma ala ya muziki kutoka afrika ya mashariki kujifunza zaidi kuhusu ala na kutengeneza ala. Ala nyingi zinatoka Kenya, Tanzania, Uganda, na nchi nyingi za afrika ya mashariki. Muziki ni muhimu sana kwa sherehe au kupitisha taarifa. Kwa mfano, muziki inatumika na harusi, mazishi, matibabu, kuweka saa, kufundisha, kufurahisha, na khadithia.


Embaire

Embaire iko ala ya kufanana na marimba na inatoka nchi ya Uganda. Kutengeneza embaire, tundu linachimbwa futi moja na nusu ya chini na urefu ni futi nane. Shina la ndizi linalazwa kwa upande pamoja wa tundu. Majani ya tembo marefu yanalazwa juu ya shina kama mto. Mbao (kutoka mbao ya ensambiya) za kufanana sehemu ya kinanda (piano) zinalazwa juu ya majani kuficha tundu. Embaire ina mbao ishirini na moja na watu wa sita hupiga embaire mara moja. Kupiga embaire, wanamuziki wanatumia fimbo/nyundo (kutoka mbao ya enzo) au mikono yao. Kwa watu wa Busoga, muziki ina uhusiano wa roho na desturi ya Mbusoga kutoa mhanga kuku kurekebisha sauti ya embaire.

Endere

Endere iko filimbi na inatoka Uganda pia. Endere ni fupi au refu na filimbi yote ina tundu la mraba nne. Endere fupi inatoka Uganda ya mashiriki na watu wa Busoga. Endere refu inatoka Uganda ya magharibi na watu wa Ankole. Kwa kawaida, endere inapigwa na mtu peke yake lakini karibuni watu wanapiga endere na ala za muziki zingine. Wachungaji walipiga endere kuita mifugo yao.

Endingidi

Endingidi ni kufanana na fidla lakini ina kamba moja. Sehemu ya endingidi inaweza kuondoshwa rahisi na watu wanaweza kuileta ala hii bila jasho. Kamba ya ala hii inatengenezwa na ufumwale ya makongo. Makongo inaotesha kabisa afrika ya mashariki. Mwanamuziki anapiga ala na upinde na inatengenezwa na ufumwale ya makongo pia. Kasha ya wazi inatumiwa kwa mwili wa ala. Kasha inajengwa na mbao kutoka mti wa settaala. Kasha ya juu inafunikwa na ngozi ya ng'ombe changa au mbuzi changa, lakini kwanza ngozi inaweka katika maji na baadaye inanyoshwa juu ya kasha. Ngozi inafungwa na nyundo na mambo juu ya kasha. Mpini ya endingidi unachongwa na mbao gumu. Mwanamuziki huweka nywele ya nyama juu ya endingidi kwa pambo. Ala hii inamalizika katika miezi tano au sita.

Ntongooli

Ntongooli (au ndongo) ni kufanana na Endingidi lakini ina kamba nane. Ala hii ina pia bakuli ya wazi kwa mwili wa ala. Bakuli inatoka kaka ya kobe na ngozi inawekwa juu ya bakuli. Mpini wa ntongooli unachongwa na mbao kama endingidi. Mtu anaanza kujenga ntongooli au endingidi na mpini. Mtu anachonga mpini kwa muda mrefu.

Kutazama wanamuziki wanapiga ala hizi...

http://www.youtube.com/watch?v=ySP3VqcwWNI
http://www.youtube.com/watch?v=Xbrxxxx6qXA

Sunday, February 15, 2009


CHAKULA CHA AFRIKA YA MASHARIKI

Wikiendi hii, niliamua kujifunza zaidi kuhusu vyakula vya Afrika. Wanawake wanapika chakula kwa kawaida, ni kufanana katika tamaduni zingine duniani. Lakini katika sehemu mbalimbali watu wa Afrika ya Mashariki wanakula vyakula tofauti.

Karibu pwani ya Kenya, watu wengi wanakula samaki, matunda, maziwa ya nazi, na viungo. Chakula cha pwani kinaathiriwa na Waarabu. Mchuzi na chapati ni mfano mzuri wa athari ya Waarabu.

chapati

Katika sehemu ya Kenya nyingine, watu hupika na vyakula huota au karibu na nyumba. Kwa mfano, maharagwe, wali, nafaka, viazi, na kadhalika. Lakini, kama jamaa wana wanyama, hawatakufa wao kwa sababu jamaa watapata zaidi kama wanyama wanaishi. Samosas, Irio, na Ugali ni milo ya afrika ya mashariki ya desturi.

Juzijuzi niliamua kupika mlo wa desturi kutoka pwani ya Kenya. Mgeni wa maalumu sana ameniunga kwa chakula cha jioni. Jina la mgeni ni Marlene Anderson na tutasoma Kiswahili pamoja. Nimepika mchuzi wa uduvi (au kamba wadogo). Kupika mlo huu, nilihitaji...

mafuta, samaki au uduvi, chumvi, pilipili manga, kitunguu, pilipili hoho, kitunguu sumu, nyanya, maziwa ya nazi, bizari, na maji ya limau.

Kuanza, nilipika kitunguu na pilipili hoho kwanza, baadaye nimeongeza kitunguu sumu na nimepika kwa dakika moja au mbili zaidi. Baada ya kitunguu sumu, niliongeza nyanya, maziwa ya nazi, bizari, maji ya limau, chumvi, na pilipili manga. Nilivyachemka vyakula kila na joto (hari) imepunguzwa na nimepika kwa dakika nane.


Pili, nimeongeza uduvi na nimepika kwa dakika kumi zaidi au hata uduvi inageuka katika rangi ya waridi. Nimeongeza wali baada ya mchuzi ulikuwa tayari. Mlo huu ni mzuri sana na kupika rahisi. Marlene na mimi tulimaliza na tumenywa chai na tumezungumza kuhsu usafiri nchini ya Kenya, mpango wa Imani, na Kitengela.


Habari Zaidi

http://www.africaguide.com/cooking.htm
http://www.mwambao.com/
http://www.africanfoods.co.uk/east-african-foods.html


Tuesday, February 10, 2009


WATU WA MAASAI

"Maasai bila ya utamaduni ni kama punda milia bila ya milia. Kama tunaacha njia ya maisha, hatua ya pili yetu tutakufa." - Kakuta Ole Maimai

Watu wa Maasai wanatambulika kwa utamaduni wao na mapambo yao. Wanatoka Kenya ya kusini na Tanzania ya kaskazini. Lakini, watasafiri kufuata mvua kwa ng'ombe zao. Wanategemea na mifugo na kilimo kuishi. Idadi ya watu wa Maasai ni kuhusu milioni nusu. Mmaasai wanasema Maa na wanaweza kugawanyika (kugawika) katika sehemu sana kama Ildamat, Ilpurko, Ikankere, Ilkaputiei, na kadhalika.


Nyumba za Mmaasai inazungukwa na Kraal. Kraal ni kama duara na inatengenzwa kutoka miiba ya acacia. Miiba yanasaidia kuzuia samba kutoka kushambulia ng'ombe yao na mifugo mingine. Nyumba zao zinatengenzwa kuonekana kama umbo wa mkate. Zinatengenezwa kutoka tope, mafimbo, majani, samadi ya ng'ombe, na mkojo wa ng'ombe. Wanawake wanajenga nyumba hizi na nyumba moja inajengika katika miezi saba mara nyingine. Manyatas na enkang ni aina mbili za kraal. Katika manyatas, wavulana wa hirimu ya kufanana wanaishi pamoja, lakini enkang yana jamaa wengi na mifugo yao.


Watu wa Maasai wana sherehe zingi kama Emuratta (Tohara), Enkipaata (kabla ya sherehe ya tohara), Enkiama (Ndoa), na kadhalika. Mapambo na nguo zinavaa katika sherehe hizi. Kwa mfano, baada ya Emuratta, wamvulana wanavaa nguo za rangi ya nyeusi. Kwa enkang e-kule (sherehe ya maziwa) wavulana wanazinyoa nywele za rangi zao. Kwa kawaida mmaasai wanahusikana na sura zao. Watavaa shanga karibu miili yao. Mikufu mizuri mikubwa inatengenezwa na shanga na wanawake watavaa hii kwa harusi yao. Wanamume wanavaa nywele kutoka simba kwa sherehe. Mmaasai watapaka rangi uso wao kwa sherehe pia au kwa sababu nyingine. Mapambo ya watu wa Maasai ni muhimu sana sawasawa na ng'ombe zao. Mapambo ni sehemu ya utamaduni wao na uhai wao.


"Nyumba inaweza kuharibika katika siku moja, nyumba ya pya inaweza kutengenza katika miezi mingi au miaka labda. Kama tunaacha njia ya maisha kutengenza maisha ya pya, itakuwa miaka ya maelfu sana."


Habari Zaidi
http://www.maasai-association.org
http://www.maasaiwomenart.net/
saharanvibe.blogspot.com/.../simply-maasai.html
http://www.gonomad.com/features/0504/maasai_women_in_kenya.html

Monday, February 2, 2009


SANAA YA PWANI

Sanaa ya Waswahili na pwani inajionyesha katika usanifu wa majengo, vyombo vya nyumba, au mapambo ya mwili. Sanaa nyingi ziliathiriwa na Waarabu kwa sababu pwani za Afrika ya Mashiriki zilitumika kwa biashara za nje. Vitu vilibadilishwa kama pembe ya ndovu, dhahabu, na viungo. Vitu hivi vilifanya miji ya Afrika ya Mashariki kuwa na biashara sana. Biashara ya pwani ilileta fedha na tamaduni zingine.


Usanifu wa majengo wa Waswahili ni mzuri sana. Majengo mengi yana maumbo ya mabombwe, mabombwe ni kufanana na jiometri. Ishara ya usanifu majengu ni milango, nyanja, minara, na kadhalika. Milango michonga mikubwa ni dalili ya utajiri. Mitindo miwili niliyogunduwa; mtindo wa kwanza uliochongwa wenye kina lakini una mabombwe machache. Mtindo wapili ulichongwa ni bila kina lakini mabombwe haya kuwa na ulinganifu. Kiti kikubwa na pambo ni mfano mzuri mwingine wa usanifu majengo. Viti vyingi vilitengenezwa na mpingo, pembe ya ndovu, mfupa, na henzerani. Majengoni, pondo kutoka mikoko zilitumiwa kujenga paa na zilikuwa na kikomo cha futi nane au kumi.


Sanaa ya pwani haikukuwa pamoja na dini kwa sababu ya athari ya Waarabu. Kwa Jumla sanaa zaidi haikuonyesha picha ya watu au wanyama kwa sababu urithi wa Mwislamu. Umbo na njia ziliazimwa kutoka Waarabu, fahirisi na hali ni asilia. Waswahili wengi wanajua kuimba, kuyaandika mashairi, kucheza, na kuyatenga majahazi. Hakuna tofauti baina ya mtu wa kawaida na Wasanii kwa sababu watu wote hujua sanaa yote.