Monday, March 9, 2009


KANGA

Kanga ni nguo ya desturi na watu wengi wa afrika ya mashariki wanazivaa kanga. Kanga ni kitambaa chenye umbo la mstatili na hiki kina mabombwe na rangi nyingi mbalimbali. Ukubwa ya kanga ni kutoka mkono katika mkono wengine wako. Urefu ni kipimio baina ya shingo yake katika goti lake. Au kipimio cha upana ni arobaini na nne inchi na kipimio cha urefu ni sitini inchi.
Kanga inavalika katika njia tofauti, kama nguo, juu ya kichwa, kuwabeba watoto, na kadhalika. Watu wanavaa kanga kusherekea uzazi, arusi, au kuomboleza. Watu wengi watapa kanga kwa zawadi. Mara nyingine kanga zanaanunuliwa kama wawili.


Methali
Kanga zinatumiwa kwa mawasiliano pia. Kanga kila ina methali au ujumbe na inasema vitu vingine bila usemi. Mifano ya methali ni...

"Liya na tabia yako usilaumu wenzako"
"Naogopa simba na meno yake, siogopi mtu kwa maneno yake"
"Amani na upendo ni ngao yangu"
"Habari ndiyo hiyo"
"Nakutakia kila la kheri"
"Mke ni tunda ni majibu kumtunza"
"Tusisahau kwetu"

Historia
Kitambaa kililetwa katika Afrika ya Mashariki kabla ya mwaka wa elfu moja mia tisa wakati wa biashara ya nje. Nguo hizi zilitoka Ulaya, Uhundi, na nchi nyingine za mashariki. Wareno walileta kitambaa chenye mabombwe kuuza kama leso. Wanawake walikata leso katika nusu na halafu walishona kitambaa kiwili tofauti kutengeneza kitambaa kipya. Kitambaa kipya kilifanana na mnyama wa kenga na jina la kenga linatoka mnyama huyu.


Sehemu za Kanga
  • Pindo ni mpaka wenye upande nne kila ya kenga
  • Mji ni mstatili wa kati na ulionyesha picha za wanyama, mimea, watu, au umbo mbalimbali
  • Jina ni usemi katika kanga na mara nyingi ni methali


Kufanga Kanga
Unafungua kangaUnachomekea upande moja chini ya mkono Unavuta upande nygine juu ya upande moja na unachomekea chini ya mkono wengine
Mwisho
Kanga ya Rais wa Amerika


Habari Zaidi
http://www.zanzibarhistory.org/kanga%20and%20Zanzibar.htm
http://www.kangausa.com/index.htm
http://www.watatu.se/index.php
http://media.humnet.ucla.edu/quarters/06s/african103c_lec1_06s/eleanor/Site/Utangulizi.html