Monday, January 26, 2009

SANAA YA UCHONGAJI YA MAKONDE
Watu wa Makonde walirithi kwa kuishi juu ya uwanda mrefu na wametoka Tanzania ya kusini au Mozambique ya kaskazini. Wameepa ukoloni kwa muda mrefu na watu wenye nguvu na wakali, mara nyingine wameitwa Mawia. Sanaa ya uchongaji imewasaidia watu wa Makonde wamechuma. Wachongaji wengi hutumia mbao laini kama mpingo. Wanachonga vitu kama kiuchumi vyupa vya kizibo, vyombo vya dawa, mitemba, mafimbo, na kadhalika.


Sanaa ya Makonde ina mitindo miwili mikuu, mitindo hii ni Binadamu na Shetani. Mtindo wa Binadamu unaonyesha umbo la asilia na watu katika sanaa hufanya kazi ya kila siku. Mtindo wa Shetani unaonyesha umbo la roho au dini. Watu wa Makonde wanaamini kwamba mchongaji alimwumba Mmakonde wa kwanza. Hadithi ni...

"Katika mwanzo, kiumbe kilitembea duniani, kiumbe hiki hakikuwa mtu au mnyama. Mara nyingine, kiumbe kilikuwa mpweke na siku moja kilipata mbao kutoka mti na kilichonga umbo. Siku ya pili umbo hili lilikuwa na uhai na likakuwa mke wa kiumbe. Mke alizaa mtoto lakini katika siku tatu mtoto akafa. Mke aliona mauti kama kitu kibaya. Kiumbe na mke walihama kutoka mto. Tena, mke alizaa mtoto mwingine na siku ya tatu mtoto akafaa tena. Walihama tena kawa uwanda mrefu. Mke alizaa mtoto wa tatu lakini muda huu mtoto aliishi na mtoto huyu alikuwa Mmakonde wa kwanza au mtu wa kwanza."


Watu wa Makonde wanaamini kuchonga ni muhimu sana kwa sababu kabla ya mtu, kulikuwa mchongaji. Sanaa ya kwanza ilionyesha umuhimu wa wanawake. Iliwakumbusha kwamba mama ndiye aliwapa uhai. Picha ya mama ilichongwa kutoka mbao ilikuwa umbo la ulinzi. Watu walileta uchongaji huu kwa safari. Leo, sanaa ya Makonde ni tofauti. Sanaa nyingine ina dhahania na inaonyesha Mungu, roho na shetani. Wasanii wa Makonde wanatumia mawazo katika uchongaji wao kama nasaba baina ya uhai na mauti au shindano baina ya uzuri na ubaya. Uchongaji si utuli na sanaa ina mwendo au inaamba hadithi.



Habari Zaidi
(Online Exhibit) http://www.makonde-museum.de/
(Article) http://findarticles.com/p/articles/mi_m0438/is_3_35/ai_98171012
http://www.caacart.com/country.php?id=10

No comments:

Post a Comment