Thursday, January 15, 2009

SANAA YA TINGA TINGA
Sanaa ya Tinga Tinga iko aina ya sanaa ya Afrika ya Mashariki. Inatoka nchi za Tanzania na Zanzibar. Sanaa chache inapelekwa nchini ya Kenya kwa sababu inapendwa na watalii. Watalii ambao hutoka nchi za Norway, Sweden, Finland, Denmark, Switzerland na Japan hasa wanapenda sanaa ya Tinga Tinga.


Eduardo Saidi Tingatinga yako mwumbaji wa sanaa ya Tinga Tinga. Tingatinga alizaliwa nchini ya Mozambique lakini alienda mjini wa Dar es Salaam katika mwaka wa elfu moja mia tisa hamsini na tano. Katika mwaka wa elfu moja mia tisa sitini na tano Eduardo Saidi alianza kuzipiga picha. Tingatina alifahamu aliweza kuchuma na picha zake. Wasanii wengi hupiga picha kuchuma na hawapigi picha kwa wenyewe. Katika mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na mbili, Eduardo Tingatinga alipigwa bunduki na polisi. Baada ya alifa, rafiki wake walianza ushirika wa chama cha Tingatinga. Chama cha ushirika hiki kiliendelea kuwa shule ya sanaa ya Tingatinga kwa wansanii wa Zanzibar, Dar es Salaam, na kadhalika. Ushirika wa Chama cha ushirika ya Sanaa ya Tinga Tinga una wanachama hamsini na makao makuu karibu na stesheni ya Morogoro katika Dar es Salaam.


Wasanii wanaendeleza kupiga Sanaa ya Tinga Tinga. Sanaa hii inatumia rangi ya baisikeli kwa mazonite zaidi. Picha ya zamani ina mahali ya nyuma wazi na inakuwa pamoja na wanyama kama simba, twiga, kifaru, ndege, na kadhalika. Sanaa ya Tinga Tinga nyingine kuhusu methali na hadithi za kale. Eduardo Tingatinga alitumia methali ya kabila ya Makua. Sanaa hii ni sanaa ya mji lakini ina picha za vijijini.

Wasanii wengine ambao hupiga picha ya sanaa ya Tingatinga ni Simon George Mpata, Jaffari Aussi, na Mikidadi Bush Bohary. Georges Lilanga Di Nyama au George Lilanga hupiga picha pia katika mtindo wa Tingatinga. Mimi ninapenda sana sanaa yake. Lilanga alizaliwa mwaka wa elfumoja mia tisa arobaini na nne. Lilanga ni Makonde na mwanzoni alijifunza kuyachonga mashina ya Kassava. Baadaye, alihama mjini wa Dar es Salaam. George alianza chama cha ushirika kinaitcho Nyumba ya Sanaa. Alijifunza zaidi kuhusu kuchonga na kuchora. Sanaa yake inaungana utamaduni ya Makonde kama shetani na ujamaa.

Watoto Wangu Wanasema Hii Siyo Bei Kubwa

4 comments:

  1. Kazi nzuri sana, sikufikiri utaweza kufanya kazi nzuri haraka hivi. asante sana.

    Sanaa ni kio cha utamaduni

    ReplyDelete
  2. Katie utakuja Jumanne? sawa kuwa na wikendi njema.

    mwalimu

    ReplyDelete
  3. Ninapenda nafasi yako, Katie :)
    Katie au mwalimu, kwa kiswahili, mtu wa Albino, unasema nini? I am looking for a politically correct way to say Albino... sipendi neno "zeru"
    Unanisaidia?
    --sarah

    ReplyDelete
  4. Jambo, ulifanya makala nzuri. Ninapenda Tingatinga na nimefanya website hii: www.tingatinga.info na www.tingatingastories.com. Labda unaweza kuangalia. Ukiwa na interest zaidi, nipelekee barua pepe. Daniel

    ReplyDelete